Karibu kwenye mwongozo wetu wa mtumiaji

Ingawa tumejitahidi kuifanya iwe rahisi sana, hapa kuna mwongozo mfupi wa kukusaidia kupitia mchakato wa kuhariri.

Panga PDF
Unganisha PDF

Unganisha PDF

Ili kuunganisha PDF mbili au zaidi, chagua hati kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox. Unaweza kupanga faili hizo kwa mpangilio unaotaka kabla ya kuziunganisha.

Unaweza pia kuunganisha baadhi ya nyaraka zilizo na nenosiri kuwa faili moja. Pakia faili ulizozichagua, shughulikia, kisha pakua faili yako iliyounganishwa. Angalia ‘Unganisha PDF'mipakakwa kila aina ya akaunti.

Gawa PDF

Gawa PDF

Ili kugawa PDF kuwa faili tofauti, chagua hati kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti zako za hifadhi za wingu kama vile Hifadhi ya Google au Dropbox. Unaweza pia kugawa hati zilizo na nywila.

Pakia faili ili kuligawa. Unaweza kugawa faili yako kwa anuwai za kurasa au kutoa kurasa zote. Pia unaweza kuunganisha anuwai zote katika faili moja ya PDF. Bonyeza kitufe cha ‘Gawa PDF’ na itakuwa tayari. Angalia ‘Gawa PDF’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Ondoa kurasa

Ondoa Kurasa

Ili kuondoa kurasa kutoka kwenye PDF moja au zaidi, pakia faili yako kutoka kwenye kifaa chako au ipakie kutoka kwenye akaunti za wingu zilizounganishwa kama vile Hifadhi ya Google au Dropbox. Unaweza pia kuondoa kurasa kutoka kwenye hati zilizo na nywila.

Utaona kielelezo kidogo cha kila ukurasa wa faili yako. Unapopakua faili nyingi, kielelezo kidogo cha kila faili kitatengwa kwa rangi tofauti. Unaweza kubonyeza kila kielelezo kidogo ili kuondoa ukurasa huo. Baada ya kubonyeza, msalaba mwekundu utaonekana juu ya kielelezo, unaonyesha kuwa ukurasa huo utaondolewa. Bonyeza kitufe cha ‘Ondoa Kurasa’ ili kupakua PDF yako iliyoshughulikiwa. Angalia ‘Ondoa Kurasa’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Dondoa kurasa

Dondoa Kurasa

Ili kudondoa kurasa kwenye faili ya PDF, pakia faili yako kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti zako za hifadhi ya wingu kama vile Hifadhi ya Google au Dropbox. Unaweza pia kuondoa kurasa kutoka kwenye hati zilizo na nywila.

Utaona kielelezo kidogo cha kila ukurasa wa faili yako. Unapopakua faili zaidi ya moja, kielelezo kidogo cha kila faili kitapakiwa kwa rangi tofauti. Bonyeza kurasa unazotaka kutoa. Chagua ikiwa unataka kuunganisha kurasa zote zilizotolewa kuwa PDF mpya au kuzipakua katika folda ya .zip. Kisha, bonyeza kitufe cha ‘Toa kurasa’. Angalia ‘Toa Kurasa’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Panga PDF

Panga PDF

Ili kupanga kurasa kutoka kwenye faili la PDF, pakia faili yako kutoka kwenye kifaa chako au ipakie moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zako za wingu kupitia Hifadhi ya Google au Dropbox. Unaweza pia kuondoa kurasa kutoka kwenye hati zilizo na nywila.

Utaona kielelezo kidogo cha kila ukurasa wa faili yako. Unapopakua faili zaidi ya moja, kielelezo kidogo cha kila faili kitatengwa kwa rangi tofauti. Kisha unaweza kuondoa au kuvuta kielelezo kidogo ili kupanga upya kurasa za PDF kama unavyotaka. Bonyeza kitufe cha ‘Panga PDF’ ili kupakua PDF yako mpya. Angalia ‘Panga PDF’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Boresha PDF
Weka alama fifi kwenye PICHA

Bana PDF

Ili ubane faili za PDF, chagua hati kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox. Pakia faili moja au nyingi. Chagua kati ya kiwango cha juu sana, cha juu, au cha kawaida cha ubanaji, kisha bofya kitufe cha Bana PDF. Kadri kiwango cha ubanaji kinavyoongezeka, ndivyo ukubwa wa faili na ubora wake unavyopungua.

Bonyeza kitufe cha ‘Punguza ukubwa wa PDF’ ili kupakua PDF yako iliyopunguzwa au uihifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘Bana PDF’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Hariri PDF
Hariri PDF

Hariri PDF

Ili kuhariri PDF yako, pakia faili yako kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Ukiwa ndani ya kionesha PDF, tumia upau wa vidhibiti wa juu kusogeza katika hati yako. Bofya aikoni ya gurudumu ili uchague mpangilio wako wa kurasa. Unaweza kuangalia ukurasa mmoja au kurasa nyingi kwa wakati mmoja. Ili kusogeza ndani au kati ya kurasa, chagua aikoni ya mkono.Tumia aikoni ya lenzi kukuza na kupunguza uonekanaji wa sehemu maalum za hati.

Ili kuongeza vipengele au maandishi kwenye ukurasa, sogeza chini hadi kwenye ukurasa unaotaka kuhariri. Chagua kutoka kwenye aikoni za Maandishi, Picha au Maumbo yaliyopo kwenye upau wa vidhibiti wa ‘Hariri PDF’ juu ya kionyeshi. Tumia kipanya chako kurekebisha ukubwa au kusogeza kipengele chochote kama unavyotaka kwenye ukurasa ule ule ulioanzishwa.

Ili kuongeza vipengele kwenye ukurasa tofauti, nenda kwenye ukurasa huo kisha chagua kipengee kipya kutoka kwenye upau wa vidhibiti. Badilisha rangi, uwazi, rangi ya mipaka, mzunguko, muundo au unene wa picha, maumbo au maandishi yako kwa kutumia upau wa sifa zao. Bofya kitufe cha ‘Hariri PDF’ ili kushughulikia faili yako.

Weka namba za kurasa

Weka namba za kurasa

Ili kuweka namba kwenye kurasa za PDF, pakia faili zako kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox. Chagua ikiwa unataka kuweka namba kwenye kurasa zote au kurasa zinazoonekana. Chagua kiwango cha kurasa unazotaka kuweka namba. Pia unaweza kuhariri nafasi ya namba yako, muundo wake (fonti, ukubwa, rangi, uwazi…) kwenye upau wa vidhibiti.

Kisha bofya kitufe cha ‘Weka Namba za Kurasa’ na pakua au uhifadhi tena kwenye wingu PDF yako iliyopatiwa namba. Angalia ukomo wa ‘Namba za Kurasa’ kwa kila aina ya akaunti.

Weka alama maalum

Weka alama maalum

Ili kuweka alama maalum kwenye faili za PDF, pakia PDF yako kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox. Unaweza kuunganisha maandishi na picha katika alama maalum, ambayo itawekwa katika nafasi ile ile kwenye kurasa zote za faili yako. Pia unaweza kubadilisha upendavyo muundo, mwelekeo na uwazi wa alama maalum hiyo.

Kisha bofya kitufe cha ‘Weka alama maalum’ na pakua au hifadhi tena kwenye wingu PDF yako yenye alama maalum. Angalia ukomo wa ‘Alama maalum’ kwa kila aina ya akaunti.

Rekebisha PDF

Rekebisha PDF

Ili kurekebisha PDF, pakia faili yako iliyoharibika au iliyo na hitilafu kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Google Drive au Dropbox. Zana yetu itajaribu kuchambua, kurekebisha au kuokoa maudhui kutoka kwenye faili yako yenye hitilafu.

Kisha bofya kitufe cha 'Rekebisha' na pakua au hifadhi tena winguni PDF yako iliyorekebishwa. Angalia ukomo wa 'Rekebisha PDF' kwa kila aina ya akaunti.

Badilisha kuwa PDF
JPG kuwa PDF

JPG kuwa PDF

Ili kubadilisha faili moja au zaidi kutoka JPG kuwa PDF, pakia picha zako kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zako za Hifadhi ya Google au Dropbox.

Chagua kama unataka PDF yako iwe katika hali wima au mlalo, na kama unataka iwe na mipaka au bila mipaka. Pia unaweza kuunganisha picha zote katika faili moja ya PDF. Kisha, pakua PDF yako au uhifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘JPG kuwa PDF’ > mipaka kwa kila aina ya akaunti.

WORD kuwa PDF

WORD kuwa PDF

Ili kubadilisha hati moja au zaidi kutoka WORD kuwa PDF, chagua hati kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti zako za hifadhi ya wingu kama Hifadhi ya Google au Dropbox.

Bonyeza ‘Badilisha kuwa PDF’ ili kubadilisha faili yako ya .docx kuwa nyaraka isiyoweza kuhaririwa. Kisha, pakua PDF yako au uihifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘Word kuwa PDF’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

POWERPOINT kuwa PDF

POWERPOINT kuwa PDF

Ili kubadilisha faili moja au zaidi kutoka PowerPoint kuwa PDF, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye wingu kupitiaHifadhi ya Google au Dropbox.

Bonyeza ‘Badilisha kuwa PDF’ ili kubadilisha faili yako ya .pptx kuwa nyaraka isiyoweza kuhaririwa. Picha na maandishi yote kutoka kwenye uwasilishaji wako wa .pptx yatawekwa kwenye faili la PDF. Kisha, pakua PDF yako au uihifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘PowerPoint kuwa PDF’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Excel kuwa PDF

EXCEL kuwa PDF

Ili kubadilisha faili moja au zaidi kutoka Excel kuwa PDF, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Bonyeza ‘Badilisha kuwa PDF’ ili kubadilisha faili yako ya .xlsx kuwa nyaraka isiyoweza kuhaririwa. Jedwali na michoro yote kutoka kwenye Excel yako itabadilishwa kuwa nyaraka ya PDF. Kisha, pakua PDF yako au uihifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘Excel kuwa PDF’mipaka kwa kila aina ya akaunti.

HTML kuwa PDF

HTML kuwa PDF

Ili kubadilisha ukurasa wa wavuti kuwa PDF, pakia picha zako kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zako za Hifadhi ya Google au Dropbox.

Bandika URL unayotaka kubadilisha kwenye kisanduku cha maandishi. Mwonekano wa awali wa hati utaonyeshwa. Unaweza kubadilisha upenavyo mwelekeo na mipaka ya hati itakayopatikana kupitia utepe wa pembeni.

Bonyeza kitufe cha ‘Badilisha kuwa PDF’. Pakua ukurasa wako wa wavuti uliobadilishwa au uihifadhi tena kwenye Wingu. Angalia ‘HTML kuwa PDF’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Badilisha kutoka PDF
PDF kuwa JPG

PDF kuwa JPG

Ili kubadilisha PDF kuwa picha ya JPG, chagua faili kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Unaweza kubadilisha PDF yako kuwa JPG au kutoa picha zote ndani ya faili ya .zip. Kisha, bonyeza kitufe cha ‘Geuza kuwa JPG’ ili kubadilisha PDF yako kuwa JPG. Angalia ‘PDF kuwa JPG’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

PDF kuwa WORD

PDF kuwa WORD

Ili kubadilisha hati moja au zaidi kutoka PDF kuwa Word, chagua hati kutoka kwenye kifaa chako au kutoka kwenye akaunti zako za hifadhi wingu kama vile Hifadhi ya Google au Dropbox.

Bonyeza ‘Badilisha kuwa Word’ ili kubadilisha PDF yako kuwa nyaraka inayoweza kuhaririwa. Kisha, pakua faili lako la .docx au uihifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘PDF kuwa Word’ mipaka kwa kila aina ya akaunti.

PDF kuwa POWERPOINT

PDF kuwa POWERPOINT

Ili kubadilisha faili za PDF kuwa PowerPoint, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye wingu kupitia Hifadhi ya Google au Dropbox.

Bonyeza ‘Badilisha kuwa PowerPoint’ ili kubadilisha PDF yako kuwa nyaraka inayoweza kuhaririwa. Picha, maandishi na michoro yote kutoka PDF yako itabadilishwa kuwa faili la PowerPoint. Unapobadilisha nyaraka yenye kurasa nyingi, kila ukurasa utawekwa kwenye slaidi tofauti ya .pptx. Kisha, pakua faili lako la .pptx au uihifadhi tena kwenye wingu. Angalia ‘PDF kuwa PowerPoint’mipaka kwa kila aina ya akaunti.

Pdf kuwa Excel

PDF kuwa EXCEL

Ili kubadilisha faili moja au nyingi kutoka PDF kuwa Excel, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Bonyeza ‘Badili kuwa Excel’ ili kubadilisha PDF yako kuwa hati inayoweza kuhaririwa. Majedwali na michoro yote kutoka kwenye PDF yako itageuzwa kuwa faili la .xlsx. Kisha, pakua faili yako ya Excel au uhifadhi tena kwenye wingu. Angalia ukomo wa ‘PDF kuwa Excel’ kwa kila aina ya akaunti.

Usalama wa PDF
Ondoa nywila kwenye pdf

Ondoa nywila kwenye PDF

Ili kuondoa nywila kutoka kwenye faili la PDF, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Kisha bofya kitufe cha ‘Fungua PDF’. Zana yetu itafungua hati yako kwa kuondoa nywila yake. Angalia ukomo wa ‘Fungua PDF’ kwa kila aina ya akaunti.

Linda PDF

Linda PDF

Ili kulinda PDF iliyo na nywila, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Chagua nywila ya mtumiaji ili kusimba fiche na kulinda PDF yako. Kisha, bonyeza kitufe cha ‘Linda PDF’ ili uweke nywila kwenye faili yako. Angalia ukomo wa ‘Linda PDF’ kwa kila aina ya akaunti.

PDF kuwa PDF/A

PDF kuwa PDF/A

Ili kubadili au kubadilisha kwa mkupuo PDF yako kuwa PDF/A, pakia hati kutoka kwenye kifaa chako au moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya Hifadhi ya Google au Dropbox.

Kisha bofya kitufe cha 'PDF kuwa PDF/A' na pakua au hifadhi tena kwenye wingu PDF yako iliyobadilishwa kwa ajili ya uhifadhi na utunzaji wa muda mrefu. Angalia ukomo wa 'PDF kuwa PDF/A' kwa kila aina ya akaunti.

Weka saini kwenye PDF

Weka saini kwenye PDF

Ili kuweka sahihi kwenye hati yako mwenyewe

Pakia hati kwenye zana yetu ya Weka saini kwenye PDF. Tia Saini. Chagua namna unayotaka kutumia saini yako kutoka kwenye utepe wa pembeni ili kuwekea mapendeleo saini yako. Unaweza kuchora saini yako, kupakia saini uliyo nayo tayari, au kusaini kwa maandishi. Unaweza pia kuweka sehemu nyingine kwenye saini yako kama vile tarehe na herufi za za mwanzo za jina lako. Pakua. Bofya kitufe cha ‘Weka saini kwenye PDF’ ili kupakua PDF yako iliyosainiwa au uihifadhi tena kwenye Wingu.

Kukusanya Saini za Kielektroniki

Ili kuunda ombi la saini, pakia hati kwenye zana yetu ya Weka saini kwenye PDF. Baada ya kupakia hati yako ya PDF, unda ombi la saini. Utapaswa kweka watia saini, kuweka sehemu za kutia saini, kubadilisha vigezo vya usalama, kisha tuma. Weka saini. Watia saini wote watapokea barua pepe yenye ufikiaji wa hati, na wataweza kuisoma na kutia saini. Pakua. Baada ya mchakato wa kutia saini kukamilika, utapokea nakala ya hati iliyosainiwa pamoja na chaguo la kupakua rekodi ya Ukaguzi. Rekodi ya ukaguzi inaweza kutumika kama ushahidi katika kesi za kisheria.

Dhana za kiteknolojia

Faili zinazolindwa na nywila

Iwapo unachakata faili lililolindwa kwa nywila, tutakuomba utusaidie kulifungua. Baada ya kufunguliwa na kuchakatwa, tunaahidi kutohifadhi nywila hii kwenye seva zetu.

Kuzungusha faili

Unaweza kuzungusha faili zako kwa kuweka kipanya juu ya faili na kubonyeza alama ya kitufe (). Lakini ikiwa unataka kuzungusha faili zaidi ya 10 kwa wakati mmoja, unaweza kufanya hivyo moja kwa moja kwenye dirisha la ibukizo litakalojitokeza. Kabla ya kufanya hivyo, utapaswa kuandaa kurasa zote ili kuzungusha zote kwa mwelekeo mmoja.

Mzunguko wa JPG kuwa PDF

Kuzungusha picha ndani ya hati ya PDF huathiri picha hiyo pekee. Baada ya hapo, utaweza kuchagua mwelekeo wa ukurasa (wima au mlalo) ukiwa na picha mpya iliyozungushwa.

Kuweka faili katika mpangilio

Faili zinaweza kupangwa kwa njia tofauti. Vuta na uachilie faili kulingana na mpangilio unaotaka; unaweza pia kupanga kwa mpangilio wa alfabeti kwa kubonyeza ikoni ya (); na pia una chaguo la kupanga kwa mpangilio wa alfabeti kinyume kwa kubonyeza ikoni ya ().

Ubanaji wa faili

Baada ya kushughulikia faili zako, utaona ukubwa wa awali wa faili na zimepunguzwa kwa asilimia gani. Kwa faili za PDF ambazo tayari zimepunguzwa ukubwa, hatuwezi kuzipunguza zaidi.

Inapakia na kuchakata

Muda wa kupakia na kuchakata faili utategemea muunganisho wako wa Intaneti na ukubwa wa faili ulizozichagua. Iwapo kivinjari kitafungwa wakati faili zako zinachakatwa, unaweza kuangalia hali ya mchakato kwenye menyu ya ‘Akaunti Yangu’, katika sehemu ya ‘Faili Zilizochakatwa Hivi Karibuni’.

Inapakua

Faili zilizozalishwa zitafutwa kwenye seva zetu baada ya muda fulani, kulingana na aina ya akaunti yako. Pia unaweza kuzihifadhi moja kwa moja kwenye akaunti zako za Google Drive au Dropbox. Unaweza kusitisha uhalali wa kiungo cha kupakulia wakati wowote unapotaka.

Inafanya kazi kutokea kwenye wingu

Huhitaji kuwa na faili unazotaka kuchakata zihifadhiwe kwenye kifaa chako. Ikiwa una Akaunti ya Google Drive au Dropbox, unaweza kupakua moja kwa moja kwenye ukurasa wetu. Mara faili zako zikishachakatwa, unaweza kuzihifadhi tena kwenye wingu. Ili kuchakata faili zilizohifadhiwa kwenye wingu, utahitaji kuingiza nywila ya akaunti yako ya wingu mara ya kwanza unapotumia kipengele hiki. Nywila zako hazitahifadhiwa kwenye mfumo wetu. Kipengele hiki ni muhimu sana unapofanya kazi kwa kutumia kifaa cha mkononi au kishikwambi.

Chagua faili za kupakia

Ili kuchagua faili kutoka kwenye kompyuta yako, unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe cha 'Chagua picha'”. Ikiwa unataka kuchagua faili zaidi ya moja kwa wakati mmoja, shikilia kitufe cha “Ctrl” huku ukibofya faili unazotaka. Kama faili zimepangwa kwa mfuatano, bofya faili ya kwanza na ya mwisho huku ukishikilia kitufe cha “Shift”. Unaweza pia kuburuta na kudondosha faili moja kwa moja kwenye eneo letu la kazi.

Masharti ya Msingi

Tunapendekeza kutumia zana zetu kupitia vivinjari vifuatavyo: Chrome, Firefox, toleo la 10 la Explorer na kuendelea, na Safari. Ukitumia Explorer toleo la 8 au 9, chaguo la kuonyesha kurasa za hati litazimwa. iLovePDF inafanya kazi tu ikiwa Javascript imewezeshwa.

Matatizo ya kiufundi

Toleo hili jipya la iLovePDF limeundwa ili liwe rahisi zaidi kutumia na tumejaribu kushughulikia matatizo yoyote ya kiufundi. Hata hivyo, ukikutana na tatizo lolote, usisite kuwasiliana nasi. Ikiwa faili haina taarifa za siri, iambatanishe kwenye barua pepe yako ili tuweze kutatua tatizo haraka zaidi. Tutafanya kila tuwezalo ili kupata suluhisho.

Lo! Kuna tatizo na muunganisho wako wa Intaneti...