Vipengele vyetu
Huna ujuzi mkubwa wa kompyuta? Haina shida. Hata kama ni mara yako ya kwanza kutumia iLovePDF, tumefanya kila kitu kiwe rahisi sana. Kiolesura chetu ni rafiki kwa mtumiaji. Zana zetu zinafahamu kazi zake, hivyo hutakumbana na matatizo yoyote.
Kilicho muhimu kwako, ni muhimu kwetu pia
Linapokuja suala la kushughulikia faili zako, ni jukumu na wajibu wetu kutoa huduma bora zaidi iwezekanavyo
Tunajitahidi kukuletea ukubwa mdogo zaidi wa faili huku tukidumisha ubora wake kuwa wa juu zaidi.
Ili kupambana na wizi wa faili, tunafuta moja kwa moja kumbukumbu zako zote ndani ya saa mbili.
Furahia matumizi bora ya muda
Tumeunda safu nzima ya zana bora ambazo zitaharakisha michakato ya hati yako
Tunakusaidia kuokoa muda wako wa thamani
Unaweza kuhariri faili zako kwa mkupuo badala ya kuhangaika nazo moja baada ya nyingine. Faili zako huchakatwa kwa kasi ya juu, hivyo hakuna haja ya kusubiri... alimradi tu uwe na muunganisho mzuri wa Intaneti.
Uhuru wa kusimamia faili zako
Panga kwa alfabeti au kinyume chake. Umesahau moja? Unaweza kuongeza zaidi, kuondoa baadhi au kuzizungusha baada ya kupakia. Kwa sababu kushughulikia faili inaweza kuwa kazi ngumu.
Uhuru wa kuchagua jukwaa lako
Endelea kufanya kazi zako kwenye kifaa chako unachokipenda. Zana zetu zinaweza kupatikana kupitia wavuti, simu za mkononi, na kompyuta
Fanya kazi kutokea kwenye wingu
Google Drive na Dropbox imejumuishwa nasi. Hii inakuwezesha kuchukua faili zako kutoka kwenye wingu na baada ya kuchakata, kuzihifadhi tena kwenye akaunti zako za hifadhi za wingu.
Hariri popote ulipo
Kwa kuwa biashara haisimami hata ukiwa safarini, unaweza kuhariri na kubadilisha PDF zako kwenye simu yako ya mkononi kupitia iLovePDF Mobile App. Inapatikana kwenye iOS na Android.
Tumia zana zetu kwenye kompyuta yako
Bana, unganisha, gawa, badilisha na hariri faili zako za PDF bila kutumia mtandao ukiwa na faragha kamili kwa kutumia iLovePDF Desktop. Chakata faili zako moja kwa moja kwenye kompyuta yako na ongeza kasi ya uhariri.
Furahia zaidi ukiwa na Premium
Wakati mwingine unahitaji kitu cha ziada kidogo tu. Boresha hali yako ya utumiaji wa iLoveIMG na uongeze ufanisi wa hati yako
Tengeneza timu
Vipengele vya Premium vinajumuisha kusimamia timu yako ili kushiriki vitendo chaguomsingi. Kuweka alama maalum iliyo na nembo ya kampuni au kuweka muundo wa namba za kurasa ni baadhi ya mifano.
Wezesha zana zako
Zipeleke zana zetu katika kiwango cha juu zaidi na kamilisha kazi zako kwa haraka zaidi kwa kuongeza uwezo wa ukubwa wa faili na idadi ya faili unazoweza kuchakata kwa mkupuo. Tunatoa eneo la kazi lisilo na matangazo na ufikiaji usio na kikomo kwa huduma zetu zote.